Rais Dkt John Pombe Magufuli amesema jumla ya shilingi bilioni 356.324 zilitumia kwa ajili ajili ya kugharamia safari za nje za viongozi mbalimbali katika kipindi cha mwaka 2013 – 2014 na 2014 – 2015.

Akilihutubia bunge Ijumaa hii mjini Dodoma, Dkt Magufuli alisema fedha hizo ni nyingi mno na zingeweza kutumika kwenye shughuli za maendeleo.

Akisoma takwimu hizo, Magufuli alidai kuwa katika fedha hizi shilingi bilioni 183.16 zilitumika kulipitia tiketi za ndege za viongozi wa serikali na taasisi zingine kwa safari za nje. Alisema posho za viongozi waliosafiri nje ziligharimu shilingi bilioni 104.552 huku mafunzo ya maafisa nje ya nchi yakigharimu shilingi bilioni 68.612.

Alidai kuwa taasisi zilizotumia fedha nyingi zaidi kwa safari za nje ni bunge, wizara ya mambo ya nje, wizara ya fedha, ofisi waziri ya mkuu, wizara ya mambo ya ndani na zingine.

Hivi karibuni Magufuli alisitisha safari za nje za viongozi wa serikali na kudai kuanza sasa zitafanyika kwa idhini yake.

Will Smith airudia Hip- Hop kwa nguvu kubwa, afunika 'Latin Grammy Awards'
TACCEO watoa ripoti ya Uchaguzi Zanzibar, waeleza kuwepo unyanyasaji wa Kijinsia, Waishauri ZEC