Mashetani wekundu, Man Utd huenda wakabadili upepo wa ajira ya meneja ambaye atakirithi kiti cha Louis van Gaal anayepigiwa upatu wa kuondoka utakapofika mwishoni mwa msimu huu.

Man Utd wanahusishwa na kubadili upepo wa ajira ya meneja, kutokana na taarifa zilizotolewa jana na gazeti la The Sun la nchini England, kuhusu uwezekano wa uongozu wa klabu ya Valencia kuwa katika harakati za kumshawishi Jose Mourinho baada ya kumtimua Gary Neville.

Mtendaji mkuu wa Man Utd, Edward Gareth “Ed” Woodward ameripotiwa kuitamani huduma ya menaja wa klabu ya Tottenham Hotspurs, Mauricio Pochettino ambaye ameonyesha uwezo mkubwa wa kuingia kwenye harakati za kuuwania ubingwa England msimu huu.

Gazeti la The Sun, limeibuka na taarifa hiyo mapema hii leo, kwa kudai kiongozi huyo wa Man Utd, anaamini Mauricio huenda akawa mtu sahihi klabuni hapo, kutokana na hitaji la kuona heshima ya mashetani wekundu inarejea.

Hata hivtyo inadaiwa kwamba Woodward, kwa sasa anafanya kazi ya ushawishi dhidi ya viongozi wengine klabuni hapo, ili kuona umuhimu wa kumuajiri meneja huyo ambaye ni raia wa nchini Argentina.

Wakati hayo yakitokea, bado inaonekana Jose Mourinho ana nguvu kubwa ya kurithishwa mikoba ya Louis van Gaal, japo fununu za kuhitajika Estadio Mestella kuendelea kushika kasi.

Slaven Bilic Amtabiria Makubwa Dimitri Payet
Bosi Wa Aston Villa Kuwatoza Faini Mashabiki