Uongozi wa klabu ya Aston Villa, umewachimba mkwara mashabiki wa klabu hiyo kwa kuweka kanuni za kuwatoza faini ya paund tano kila mmoja, endapo watatoka uwanjani kabla ya mchezo kumalizika.

Uongozi wa klabu hiyo ya Villa Park, wamepitisha sheria hiyo baada ya kuchoshwa na tabia za mashabiki wao aambazo zilijitokeza katika michezo ya hivi karibu za kutoka uwanjani kabla ya filimbi ya mwisho kipulizwa, kwa kigezo cha kutopendezwa na kile wanachokiona zaidi ya kuendelea kupoteza point tatu muhimu.

Sheria hiyo imepangwa kuanza kesho, wakati wa mchezo wa ligi kuu ya soka nchini England, ambapo Aston Villa watakua wenyeji wa mabingwa watetezi Chelsea katika uwanja wa Villa Park.

Mbali na sheria hiyo kuwabana mashabiki ambao watatoka uwanjani kabla ya kipyenga cha mwisho, pia uongozi wa klabu hiyo umeweka sheria nyingine ya kumkata paund moja kila shabiki ambaye ataondoka uwanjani kabla ya kipindi cha kwanza hakijamalizika.

Maamuzi ya kupitishwa kwa sheria hizo, yamepewa msukumo mkubwa na mmiliki wa klabu ya Aston Villa, Randy Lerner ambaye mara zote alionyesha kuchikizwa na kuona sehemu za uwanja zikibaki wazi, ili hali mwanzoni mwa mchezao zinakua zimejaa.

Woodward Amkataa Kiaina Jose Mourinho
Ayestaran: Nisingeweza Kuwa Hapa Kama Gary Hakunipendekeza