Bodi ya Ligi Kuu (TPLB) ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imepanga mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Young Africans dhidi ya JKT Ruvu, sasa utachezwa Oktoba 26, 2016 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar s Salaam.

Pamoja na mchezo huo, imefanya mabadiliko katika baadhi ya ya michezo ya Ligi Kuu ya Vodacom kama ifuatavyo ambako Mwadui na Azam sasa utachezwa na Novemba 9, 2016 siku ambayo Prisons itaikaribisha Simba kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya. Novemba 10, kutakuwa na mchezo kati ya Young Africans dhidi ya Ruvu Shooting jijini Dar es Salaam.

Kadhalika Young African na Mtibwa sasa utachezwa Oktoba 13, 2016 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati Kagera Sugar itacheza na Azam Oktoba 28, 2016 kwenye Uwanja wa Kaitaba mjimi Bukoba huku Young Africans dhidi ya Mbao utapigwa Oktoba 30, 2016 jijini Dar es Salaam wakati Toto Africans na Mtibwa Sugar watakutana Oktoba 30, 2016 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.

Mtibwa Sugar na Mbeya City itachezwa Novemba 7, 2016 kwenye Uwanja wa Manungu huko Mvomero,  mkoani Morogoro wakati Mwadui na Majimaji itachezwa tarehe hiyohiyo huko Shinyanga kwenye Uwanja wa CCM Kambarage wakati Oktoba 7 kutakuwa na mchezo kati ya Mbeya City na Stand United kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.

NEC Yazindua Programu ya utoaji wa elimu ya mpiga kura mashuleni
Kilimanjaro Queens Neema Tupu