Kikosi cha Young Africans kimerejea jijini Dar es salaam kikitokea jijini Mwanza baada ya kumaliza mchezo wake wa Ligi Kuu Tanznaia Bara dhidi ya Kegera Sugar uliopigwa jana Jumapili (Novemba 13), katika Uwanja wa CCM Kirumba.

Mchezo huo ulishuhudia Young Africans ikiendelea wimbi la ushindi kwa kuifunga Kagera Sugar iliyokua nyumbani bao 1-0, na kufikisha alama 23 kwenye msimamo wa Ligi Kuu.

Bao pekee na la ushindi la Mabingwa hao wa Tanzania Bara lilipachikwa wavuni na Mshambuliaji kinda Clement Mzize dakika ya 18, akiunga kwa kichwa Krosi iliyopigwa na Kiungo Feisal Salum ‘Fei Toto’.

Kurejea jijini Dar es salaam kwa Young Africans, ni sehemu ya kuanza kujiandaa na mchezo ujao wa Ligi Kuu dhidi ya Singida Big Stars, utakaopigwa Alhamis (Novemba 17), Uwanja wa Benjamin Mkapa majira ya saa moja usiku.

Young Africans inaongoza msimamo wa Ligi Kuu kwa kufikisha alama 23 sawa na Azam FC iliyozidiwa mabao ya kufunga na kufungwa, huku Simba SC ikishika nafasi ya tatu kwa kuwa na alama 21.

Simba SC, Young African zoambwa kupambana CAF
Biden, Xi Jinping, Sunak uso kwa uso mkutano wa G20