Kocha Mkuu wa Klabu ya Young Africans Nasriddıne Nabi amesema kazı kubwa anayoifanya hivi sasa ni kuiongezea makali safu yake ya ushambuliaji ili kuweza kufunga mabao mengi zaidi.

Nabi ametoa kauli hiyo huku kikosi chake kikiwa kwenye maandalizi ya mwisho kabla ya mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya awali wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Rivers United ya Nigeria.

Kocha huyo kutoka nchini Tunisia amesema tangu walipomaliza Wiki ya Mwananchi, wamekua na maandalizi kabambe ya kujiwinda na mchezo huo utakaochezwa Jumapili (Septemba 12), Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaaam.

Amesema jambo kubwa kwa sasa anahakikisha safu yake ya ushambuliaji inakua na makali ya kutisha, ili kufanikisha mpango wa kupata mabao mengi kwenye mchezo huo, ili kujirahisishia kazi kwenye mchezo wa mkondo wa pili ambao utachezwa nchini Nigeria mwishoni mwa juma lijalo.

“Tumekuwa na maandalizi mazuri tangu kumalizika wiki ya kilele cha Wananchi, tumefanya mazoezi ya kutosha na mechi mbili za kirafiki ambazo zimesaidia kupata picha halisi ya kikosi hasa katika mchezo uliombele yetu karibu idara zote zipo sawa ulinzi na hata kiungo ispokuwa bado kuna kitu nataka kuongeza kwenye umaliziaji lengo ni kufunga mabao mengi zaidi.

Juma lililopita Young Africans ilicheza mechi dhidi ya Pan Africans na Friends Rangers kambini kwao Avic Town Kigamboni jijini Dar es salaam, ikiwa ni sehemu ya Programu ya kuelekea mchezo dhidi ya Rivers United.

Young Africans yasajili 28 Kimataifa
TAFIRI yatakiwa kufanya kazi yenye tija sekta ya uvuvi