Young Africans itaanza kurusha karata yake kwenye michuano ya Ligi Ya Mabingwa Barani Afrika 2021/22 kwa kucheza dhidi ya Rivers UTD ya Nigeria.

Hilo limefahamika baada ya Shirikiasho la Soka Barani Afrika kupanga ratiba ya michezo ya hatua ya awali kwa mfumo wa kuchezesha Droo.

Young Africans wataanzia nyumbani kati ya Septemba 10-12 na mchezo wa mkondo wa pili utachezwa kati ya Septemba 17-19.
nchini Nigeria.

Simba SC itasubiri hadi mzunguuko wa pili hatua ya mtoano na itaanzia ugenini.

Mshindi kati ya Jwaneng Galaxy (BOTSWANA) na Espérance FC du 5ème Arrondissement (JAMHURI YA AFRIKA YA KATI ) atacheza dhidi ya Mabingwa hao wa Tanzania Bara.

Mchezo wa mkondo wa kwanza utachezwa kati ya Oktoba 15-17, na mchezo wa mkondo wa pili utapigwa Dar es salaam kati ya Oktoba 22-24.

Makapu awaaga Wanachama, Mashabiki Young Africans
Serikali yatoa ufafanuzi Daktari aliyeanguka