Rapper Young Killer Msodoki kutoka jiji la Miamba, Mwanza, amepanga kuachia kanda mseto (mixtape) yake itakayobeba nyimbo 14.
Young Killer ameiambia Bongo5 kuwa nyimbo hizo 14 ni zile ambazo alizifanya kabla hajaanza kujulikana kwenye mkondo mkuu wa muziki hapa Bongo. Kupitia Kanda mseto hiyo, mashabiki watamfahamu Young Killer anaechipukia habla ya ‘Dear Gambe’.

Hivi ndivyo alivyosema:

“Kikubwa kabisa namshukuru mwenyezi Mungu kwakuwa yeye ndo mweza wa kila kitu. Nadhani wiki hii ndio wiki ambayo nitaufungua mwaka kwa ujio wangu mpya ambao utakuja kuambatana na mixtape ambayo itakuwa na ngoma 14 ambazo nimefanya zamani kabla sijatoka kwenye muziki, kabla ya hata Dear Gambe haijasikika,”

“Kwahiyo mashabiki wasubirie mixtape ya Msodoki the Son. Kikubwa kabisa najaribu kuwaonyesha uwezo niliokuwa nao hata kabla sijatoka, waweze kunijua zaidi uwezo wangu. Pia nawapa moyo hata wale underground kwamba ni vizuri pia kuzipima ngoma zao wanazofanya kabla hawajapata nafasi na pia wazitunze ili baadaye waje kuzitumia katika biashara zao.”

Chanzo: Bongo5

Fabio Capello Akubali Kubwaga Manyanga Urusi
Hasheem Thabeet Ashauriwa Kusaka Timu Uturuki