Chuo cha Uhasibu Nchini, kimefanya Mahafali ya 21 kwa ngazi mbalimbali za Elimu ya juu yaliyohudhuria na wadau mbalimbali wa Serikali, sekta ya Elimu na binafsi ambapo mgeni rasmi katka mahafali hayo aliyehudhuria Kwa niaba ya Waziri wa Fedha ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Elijah Mwandumbya .
Katika hotuba ya mgeni rasmi iliyosomwa na Katibu Mkuu huyo amesema anaipongeza Taasisi hiyo Kwa kuifikia mahali ya 21, lakini pia kuwa na mahafali ya kwanza ya Masters katika kampasi ya Dar es salaam na kufurahi kupewa heshima ya kuwa mgeni rasmi.
Aidha amepongeza Taasisi hiyo kwa kuanzisha mashindano na mawazo bunifu Kwa wanafunzi, kuwa na vijana wenye vipawa na wenye uwezo wa kutoa huduma kupitia vipaji vyao, vinavyowapatia vipato na kuwaasa wahitimu kuendelea kuwa wabunifu ili waweze kujiajiri.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Nchini, Prof. William Pallangyo amesema jumla ya Wanachuo 7,252 wamehitimu, Wanawake wakiwa ni 3974 sawa na asilimia 54.7 na Wanaume 3269 sawa na 45.5.