Zaidi ya watu milioni 1, wameyakimbia makazi yao nchini Somalia tangu mwaka 2021 kutokana na ukame, huku ikikadiriwa kuwa watoto milioni 1.5 wenye umri wa chini ya miaka 5 wanakabiliwa na utapiamlo na 386,400 wakihitaij tiba dhidi ya ugonjwa huo ili waweze kuishi.

Kufuatia hali hiyo, Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura (OCHA), Martin Griffiths ametoa dola milioni 10 kutoka Mfuko wa dharura wa UN, CERF ili kuongeza kasi ya utoaji wa misaada ya dharura nchini Somalia, ambay iliyo na ukame kwa kipindi cha miaka 40.

Taarifa ya OCHA, iliyotolewa leo jijini Geneva-Uswisi na New York-Marekani imesema msaada huo unakuja kufuatia kutangazwa kwa viwango vya juu vya ukosefu wa uhakika wa chakula kuwahi kufikiwa tangu mwaka 2017.

Watu 213,000, wako katika mazingira yanayofanana na kukumbwa na baa la njaa, huku milioni 7. 8 kati yao wakiwa hawana uhakika wa chakula ambapo Griffiths amesema, “Muda unakwisha kwa watu wa Somalia, iwapo hatutachukua hatua sasa, muda utakwisha pia kwa watoto wenye utapiamlo ambao wanaweza kufa.”

Mtoto mwenye utapiamlo akipatiwa matibabu, Picha na Daily Ummah/UNICEF

Fedha hizo zilizotolewa, zitasaidia mashirika yanayotoa misaada ya kibinadamu kupata vyakula na watendaji kwa haraka iwezekanavyo ili kuepusha janga lililoikumba nchi ya nchi hiyo ya pembezoni mwa Afrika.

Hata hivyo, Griffiths amesema hilo si jawabu linalotosheleza, na kwamba inahitajika kuchukuliwa kwa hatua na kuhamasisha rasilimali ili ikuzuia njaa isiendelee kuathiri maisha ya raia wengi walio katika hali mbaya.

OCHA inasema kwa nusu ya kwanza ya mwaka huu wa 2022, watoa misaada ya kibinadamu walifikia watu milioni 4 na kwamba fedha kutoka CERF zitaendelea kuimarisha juhudi zao ili kupeusha janga hilo.

Halmashauri zatakiwa kutekeleza agizo la Rais
Shambulio Hotelini lauwa zaidi ya watu 10