Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bosi ya Ligi Kuu ‘TPLB’ imekuta na hatia Afisa habari wa klabu ya Azam FC Thabit Zacharia (Zaka Zakazi) kufuatia kauli aliyoitoa katika vyombo vya habari na andiko lake kupitia Mitandao ya Kijamii baada ya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Tanzania Prisons.

Azam FC ilipoteza kwa kufungwa 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya juma lililopita, huku Zaka Zakazi akiwatupia lawama waamuzi kwa kudai hawakuitendea haki timu yao.

Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi kupitia kikao chake cha Oktoba 04, imefikia maamuzi ya kumfungia Zaka Zakazi Kwa Kipindi cha Miezi mitatu pamoja na kumtoza Faini ya Shilingi laki Tano (Tsh 500,000).

Taarifa iliyotolewa na Bodi ya Ligi Kuu ‘TPLB’ imeeleza kuwa Zaka Zakazi amekumbwa na adhabu hiyo Kwa kosa la kuwashutumu Waamuzi wa mchezo kati ya Tanzania Prisons dhidi ya Azam FC Kupitia Mitandao yake ya Kijamii.

Taarifa hiyo imeendelea kueleza kuwa Zaka Zakazi alifanya kosa hilo huku akifahamu Klabu yake ilikua imeshatumia njia sahihi ya kikanuni kwa kuandia barua Bodi ya Ligi Kuu ‘TPLB’ kuhusu malalamiko kwa waamuzi waliochezesha mchezo dhidi ya Tanzania Prisons.

Maafisa wa Al Hilal wahofia mbinu za Nabi
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Octoba 06, 2022Â