Wananchi visiwani Zanzibar na wenzao wa Bara, leo wameungana kusherehekea kumbukumbu ya miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar huku gwaride maalum likifanyika visiwani humo na kuhudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu wa Taifa wakiongozwa na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Shein na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli.

Hata hivyo, wananchi waliohudhuria walitumia nafasi hiyo kumfikishia ujumbe rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Magufuli kuimulika Zanzibar na kufanya kazi ya kutumbua ‘majipu’ kama alivyofanya kwa upande wa Bara.

“Zanzibar majipu yapo… Zanzibar Majipu yapo… Zanzibar Majipu yapo’, ndio salamu za mapokezi zilizosikika kutoka kwa umati uliohudhuria wakati Rais John Magufuli alipokuwa akiingia uwanjani hapo.

Msamiati wa kutumbua majipu aliutoa rais Magufuli wakati akifungua rasmi Bunge na kueleza kuwa atapambana na wezi na mafisadi ambao aliwaita ‘majipu’.

CCM wamjibu Maalim Seif, Watahadharisha 'nguvu ya umma'
Sherehe Kichaa: Maelfu watembea nusu watupu kuadhimisha 'No Pants Day'