Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali imelitangaza zao la michikichi kuwa zao kuu la sita la biashara linalotarajiwa kuinua uchumi Taifa.

Awali, kulikuwa na mazao makuu matano ya biashara nchini ambayo ni Korosho, Tumbaku, Pamba, Kahawa na Chai, ambayo yanategemewa na Taifa kukuza uchumi.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Mwakizega Wilayani Uvinza Mkoani Kigoma.

Amesema kuwa baada ya Serikali kupata mafanikio katika mazao ya Korosho, Tumbaku, Pamba, Kahawa na Chai, sasa imeamua kufufua zao la michikichi mkoani Kigoma ili lianze kuzalishwa kwa wingi na kuongeza pato la Taifa.

“Tulianza na mazao matano, baada ya wakulima wake kupata faida sasa tumehamia katika mazao mengine likiwemo la michikichi,” amesema Majaliwa.

Aidha, ameongeza kuwa Serikali imeamua kulipa kipaumbele zao hilo kwa lengo la kumaliza tatizo la upatikanaji wa mafuta ya kula nchini.

Hata hivyo, amesema kuwa kwa mwaka Serikali inatumia zaidi ya sh. bilioni 600 kuagiza mafuta ya kula nje ya nchi, hivyo ufufuaji zao hilo utaliwezesha Taifa kuzalisha mafuta ya kutosha.

 

Everton kuvuruga mipango ya Chelsea
Robert Lewandowski awekewa vikwazo FC Bayern Munich