Kinara wa Azimio na upinzani nchini Kenya, Raila Odinga asema atazindua zoezi la kukusanya sahihi za wakenya za kutokuwa na imani na serikali ya Kenya Kwanza siku ya Ijumaa Julai 7, 2023.

Odinga ameyasema hayo hii leo Julai 4, 2023 na kuongeza kuwa hatua hiyo inatokana na Wakenya wengi kuchoshwa na Serikali kutokana na kuwakandamiza kwa mambo mengi ikiwemo kupanda kwa gharana za maisha na lundo la kodi.

Aidha, Odinga pia amewakata Wakenya wengi walio na mapenzi mema na Taifa hilo, kujitokeza kwa wingi siku ya Sabasaba uwanja wa Kamukunji ili kushiriki zoezi hilo.

Hatua hii inakuja ikiwa ni muda mfupi tangu Muungano wa Matatu (daladala), nchini kutangaza kupandisha nauli kwa usafiri wa umma kwa asilimia 30 kuanzia hapo kesho Jumatano Julai 5, 2023. ukisema umechukua hatua hiyo kufuatia hatua ya Serikali kupandisha bei ya mafuta.

Usajili Azam FC wamshutua Feisal Salum
Liverpool kuibomoa Southampton