Ushangiliaji wa kiungo mshambuliaji wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC Bernard Morrison baada ya kufunga bao la tatu kwenye mchezo wa Simba Super Cup dhidi ya Al Hilal ya Sudan, umepokelewa tofauti na Afisa Habari wa Ruvu Shooting Masau Bwire.

Morisson alishangilia bao hilo kwa kuweka mpira sehemu zake za siri, kitendo ambacho kiliwafurahisha mashabiki waliokua wanaufuatilia mchezo huo Uwanja wa Benjamin Mkapa, na wale waliokua wanautazama kupitia Runinga.

Masau ameonesha kupokea tofauti ushangiliaji huo kwa kuandoka ujumbe kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii, akihisi mshambuliaji huyo anajichulia mabalaa.

Masau ameandika: Aombacho mtu hupewa. Huyu bingwa naona anaomba kutune kama mpira wa miguu. Kwa kuwa Mungu si Athumani, siku ombi lake likijibiwa, asipige kelele!

Au wadau mnasemaje?

Inafikiriwa kuwa Morrison alishangilia bao lake kwa njia ile, ikiwa ni jibu kwa baadhi ya wadau wa soka waliokua wanamzungumza vibaya kufuatia tetesi zilizosambaa kwa kasi kuhusu maradhi ya ‘Mshipa wa Ngiri’ ambayo yalitajwa kuwa kikwazo kwake cha kushindwa kuwa sehemu ya kikosi cha Simba wakati wa michuano ya Kombe la Mapinduzi.

Jeshi la polisi lafunguka kifo cha dereva wa lori
Bumbuli: Nililipa faini na pay slip nilipeleka TFF