Klabu ya AC Milan imeonyesha kuwa tayari kuingia gharama, ili kuhitimisha mpango wa kumsajili mshambuliaji kutoka nchini Hispania na klabu ya Real Madrid  Alvaro Morata.

Gazeti la michezo la nchini Italia (Gazzetta dello Sport) limeanika wazi mpango huo wa AC Milan, ambao wamedhamiria kukisuka sawa sawa kikosi chao kwa ajili ya msimu ujao wa ligi ya Sirie A.

Gazeti hilo limeibuka na kichwa cha habari kinachoeleza “BAADA YA KUJARIBU KWA LEONARDO BONUCCI WA JUVENTUS SASA NI ZAMU YA MORATA

AC Milan inatajwa kumuandalia mkataba mnono Morata ambao utamuwezesha kulipwa mshahara wa Euro milioni 10 hadi 12 kwa mwaka, huku ada yake ya uhamisho ikitarajiwa kufikia Euro milioni 70.

Klabu hiyo ya mjini Milan imepata nguvu ya kujitosa kwa mshambuliaji huyo ambaye aliwahi kuitumikia Juventus FC, kabla ya kurejea Real Madrid mwishoni mwa msimu wa 2015/16, baada ya kuona Man Utd wamejiondoa kwenye harakati za kumsajili.

Man Utd wamesitisha mpango wa kumuhamishia Morata Old Trafford, kuafutia harakati zao za kumnasa mshambuliaji kutoka nchini Ubelgiji Romelo Lukaku kukamilishwa juma lililopita.

Haji Manara Na Wenzake Waachiwa Huru
Chelsea yamtaka Aguero

Comments

comments