Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na wananchi umefanya msako mkali wa kumtafuta maeneo ya Matundasi, Mji mdogo wa Makongolosi kwa kumtafuta mtuhumiwa katika tukio la mauaji ya Adam Jacob (31) mchimbaji na mkazi wa kitongoji cha Kasakalawe.

Akitoa taarifa hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya SACP Ulrich Matei amesema kuwa kupitia msako huo wamefanikisha kumkamata mtuhumiwa Devi Abraham Mwambebule (32) mkazi wa Matundasi aliyehusika na mauaji hayo.

Aidha Kamanda Matei amesema mtuhumiwa amehojiwa na kukiri kosa kuhusika katika tukio.

Upepelezi unaendelea na mara baada ya upelelezi kukamilika mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.

Mchele wa Morogoro kuuzwa kimataifa
Hakuna kuingia serikalini bila chanjo