Saa chache baada ya kutangazwa kuwa meneja wa muda wa kikosi cha klabu ya Valencia, Francisco Martín “Pako” Ayestarán Barandiarán amefichua siri ya kukabidhiwa jukumu hilo kwa kumtaja aliyekua bosi wake katika benchi la ufundi, Gary Neville.

Ayestaran aliyekua msaidizi wa Neville, amesema anaamini maamuzi yaliyochukuliwa na viongozi wa ngazi za juu ya kumteua kuwa meneja wa muda, yametokana na baraka alizoachiwa na bosi wake.

Akizungumza mara baada ya kuthibitishwa kuwa mkuu wa benchi la ufundi huko Estadio Mestella, Ayestaran amesema kabla ya Neville kuondoka klabuni hapo alikutana na viongozi na anaamini alipendekeza kuteuliwa kwake.

Hata hivyo amesisitiza kuifanya kazi yake ipasavyo, ili kutimiza jukumu alilopewa kwa kuaminiwa na viongozi la kuiwezesha Valencia kuwa na matokeo mazuri hadi mwishoni mwa msimu huu.

“Nisingeweza kuwa hapa kama Gary hakunipendekeza.” Alisema Ayestaran

“Nilizungumza nae kabla sijakubali uteuzi huu na alinitaka kukubali bila hiyana yoyote kutokana na kuamini uwezo wangu.”

“Naamini aliwaambia viongozi nina uwezo na hakutokua na shaka katika mipango iliyowekwa klabuni hapa hadi mwishoni mwa msimu huu.” Aliongeza mbadala huyo wa Gary Neville.

Ayestaran ambaye ni raia wa nchini Hispania, alianza kazi klabuni hapo sambamba na Neville mwezi januari mwaka huu.

Bosi Wa Aston Villa Kuwatoza Faini Mashabiki
Herve Renard Aipeleka Morocco AFCON 2017