Rais wa chama cha soka nchini Misri, Hani Abou Rida amejiuzulu na kikosi kizima chaufundi kufuatia kutolewa mapema kwa timu hiyo kitu ambacho hakikutarajiwa katika michuano ya soka ya kombe la mataifa ya Afrika nchini Misri.

Katika taarifa iliyotolewa na chama cha soka nchini Misri, imesema kuwa viongozi hao walipaswa kujiuzulu kwani wamewaangusha pakubwa mashabiki wa soka, hivyo hata waliobaki wametakiwa kujiuzulu.

Matokeo ya mechi ya Jumamosi yalipelekea mshtuko mkubwa kwa mashabiki wapatao 75,000 katika uwanja wa Cairo pamoja na wananchi wa Misri kwa jumla wakishuhudia timu yao iliyokuwa ikipewa nafasi kubwa ikichapwa bao 1-0 na Afrika kusini.

Aidha, Rida ameongoza chama cha soka cha Misri tangu mwaka 2016, katika muda wote chama hicho kimegubikwa na misukosuko ikiwa ni pamoja na timu kutolewa mapema katika michuano ya kombe la dunia 2018 katika hatua ya makundi.

Uwanja wa soka wa kimataifa wa Cairo uliokuwa umefurika watu na ngoma na matarumbeta yalikuwa kimya baada ya mchezo huo huku baadhi ya mashabiki wakibubujikwa machozi ya kutoamini kilichotokea.

Matokeo hayo yaliwaduwaza wengi  kwa kushindwa kuamini kilichotokea baada ya kipigo cha dakika za mwisho kutoka kwa timu ya taifa ya Afrika Kusini, Bafana bafana.

 

Video: Msaidizi wa Membe adaiwa kutekwa Dar | Askofu afunguka kuhusu utekaji
Msaidizi wa Membe adaiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha

Comments

comments