Joe Jackson ambaye ni baba mzazi wa marehemu Michael Jackson alipata ajali ya gari jana katika eneo la Las Vegas alipokuwa akiendelea na safari yake.

Kwa mujibu wa TMZ, mashuhuda wa ajali hiyo wameeleza kuwa walimuona mzee Jackson mwenye umri wa miaka 88 akitoka kwenye gari lake lililopata ajali akiwa anashikilia kifua kuashiria alikuwa anahisi maumivu.

Mashuhuda hao walieleza kuwa  mzee Joe alikaa kwa muda mrefu katika eneo la karibu na ajali hiyo na baadae kukimbizwa hospitalini.

Hata hivyo, saa chache baada ya tukio hilo, taarifa ya maendeleo ya afya yake ilitolewa kupitia akaunti yake ya Twitter.

“Bwana Jackson alipata ajali ndogo, lakini hakuna kibaya kilichotokea kwake. Hakupata hata majeraha na yuko salama, buheri wa afya. #teamJackson,” inasomeka taarifa hiyo.

Kupitia tovuti yake binafsi, mzee Jackson alieleza kuwa msaidizi wake ndiye aliyepata jeraha kwenye kidole gumba. Alisema ajali hiyo ilisababishwa na gari moja kutokea ghafla mbele ya gari lao.

Diamond asema 'neno' kuhusu agizo la Rais kwa wanafunzi watakaopata mimba
?Live: Kamati ya katiba na sheria bungeni yakutana kufanya marekebisho ya sheria