Uongozi wa klabu ya Bordeuax ya nchini Ufaransa, umedhamiria kumsajili moja kwa moja beki wa pembeni wa klabu ya Arsenal, Mathieu Debuchy baada ya kumtumia kwa mkopo.

Le Parisien, wamejipanga kuwasilisha ofa ya kumuhamisha moja kwa moja beki huyo mwenye umri wa miaka 30, kufuatia kiwango chake kuwaridhisha tangu alipoanza kuwatumikiwa mwanzoni mwa msimu uliopita.

Debuchy, amekua na wakati mgumu wa kuwania nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha The Gunners, kufuatia uwepo wa beki kutoka nchini Hispania Hector Bellerin ambaye ameonyesha kuimudu nafasi ya mlinzi wa kulia.

Debuchy, alipoteza nafasi yake katika kikosi cha kwanza, mara baada ya kuumia bega msimu wa 2014-15, na nafasi yake ilipokabidhiwa kwa Bellerin, haikuwa rahisi tena kumshawishi Arsene Wenger kumrejesha kundini.

Beki huyo kutoka nchini Ufaransa ambaye alisajiliwa na Arsenal mwaka 2014 akitokea Newcastle Utd kwa ada ya Pauni milioni 10, amesafiri na kikosi cha The Gunners kuelekea Marekani kwa ajili ya kambi ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi, na anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi kitakachocheza mchezo wa kirafiki dhidi ya nyota wa ligi ya Marekani (MLS All Stars).

Mwishoni mwa juma lililopita, alicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Lens, ambapo Arsenal walilazimisha matokeo ya sare ya bao moja kwa moja.

Mwendo Kasi kuburuzwa mahakamani kwa wizi wa nauli, madereva nao kukiona
Afrika Kuwa Na Timu Saba Fainali Za Kombe La Dunia 2026