Nchi za Brazil na Argentina, zinakusudia kushirikiana kiuchumi ikiwemo kuwa na sarafu moja ambayo itakuwa inatumika katika kanda nzima ya Amerika Kusini.

Hayo yamebainishwa na marais wa nchi hizo Luiz Inacio Lula da Silva wa Brazil na Alberto Fernandez wa Argentina huko mjini Buenos Aires.

Rais wa Brazili, Luiz Inacio Lula da Silva (kulia), akiwa na Rais wa Argentina, Alberto Fernandez. Picha ya Maira Erlich | Bloomberg.

Kupitia taarifa yao, Viongozi hao wamesema wazo la kutumia sarafu moja lilitolewa na Fernando Haddad mwaka jana (2022), ambaye kwa sasa ni waziri wa fedha wa Brazil.

Aidha, Rais Lula ameitembelea Argentina katika ziara yake ya kwanza tangu kuapishwa kwake na kuendeleza utamaduni ambao umekuwepo wa kumtembelea mshirika mkubwa wa kwanza wa kibiashara wa nchi yake.

Saba mbaroni tuhuma za mauaji ya Hakimu
Fiston Mayele awaita Wananchi kwa Mkapa