Mipango ya wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya kimataifa, Young Africans  kujinasua mkiani mwa msimamo wa Kundi A la michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika imepata nguvu zaidi baada ya ombi lao la kubadilisha siku ya mchezo wao na Medeama kukubaliwa.

Shirikisho la Soka Barani Afrika limebadili tarehe ya mchezo wa Young Africans dhidi ya Medeama kutoka siku ya Ijumaa ya tarehe 15 Julai na sasa kuchezwa Jumamosi ya tarehe 16 Julai.

Awali ikumbukwe CAF waliwakatalia Young Africans  kubadili siku ya mchezo wa pambano lao dhidi ya TP Mazembe kwa kuwa walichelewa kuwasilisha ombi lao. Kwa kulitambua hilo, Yanga walituma ombi lao mapema kuomba kubadilishwa kwa mchezo wao dhidi ya Medeama na CAF kuwakubalia hii leo.

Pambano kuchezwa Jumamosi kutatoa fursa kwa Young Africans kupata nguvu ya mashabiki zaidi kulinganisha na tarehe ya awali ya Ijumaa.

Young Africans iliyofungwa na TP Mazembe bao 1-0 katika mchezo uliopita na kujikuta wakiburuza mkia katika kundi A baada ya kupoteza michezo miwili mfululizo.

Makonda Awaapisha Wakuu Wa Wilaya Mkoa Wa Dar es salaam
UZINDUZI RASIMI WA TAASISI YA MARIDHIANO YA KIDINI WAJA