Rapa Chid Benz ameendeleza tambo za hip hop akidai kuwa ndiye msanii mkali wa michano zaidi Tanzania na kwamba uwezo wake haufananishwi na Mfalme wa Kaskazini, Joh Makini.

Chid Benz amefunguka kwenye The Playlist ya 100.5 Times Fm kuwa ingawa anaheshimu uwezo mkubwa wa Joh Makini, bado anaamini kuwa hawezi kulinganishwa naye katika michano.

“Huwezi kunifananisha mimi na Joh Makini by the way,” Chid alimwambia Mtangazaji wa The Playlist, Lil Ommy. “Like nikisema niongelee ukweli. Yaani kama hapa akae hapa Joh… me I respect him as ana artist. But mule ule mimi nafanya yeye alikuwa bado. Kwahiyo kuhusu suala la kuchana na ukali, Chid is the best,” aliongeza.

Joh Makini

Joh Makini

Chid ambaye hivi karibuni ameachia wimbo ‘Chuma’ aliomshirikisha Raymond wa WCB alieleza kuwa ingawa yeye ni rapa mkali zaidi, amekuwa akiwekwa kando na ‘washika dau’ huku wasanii wengine wakitengenezwa na kupata njia nzuri zaidi kibiashara.

Hata hivyo, Chid Benz alikana kumuweka Joh Makini kwenye kundi la wasanii ambao alidai wametengenezwa.

“Sijasema Joh Makini ametengenezwa, nimesema kuna wasanii wametengenezwa,” alisema.

Chid ambaye hujiita King Kong anayeshikilia rekodi ya rapa aliyeshinda tuzo nyingi za KTMAs, alitamba kurudisha heshima ya jina lake kwa kishindo baada ya kufanikiwa kujiondoa kwenye matumizi ya dawa za kulevya.

Kwa upande wa Joh Makini, amekuwa miongoni mwa wasanii wa kwanza wa hip hop Tanzani akuipeleka rap ya Tanzania nje ya Afrika Mashariki na kufanya collabo na wasanii wakubwa Afrika kama AKA, Chidnma na wengine.

Chadema waanza ‘majaribu’, wagawa bendera za Ukuta
Video: Majambazi hatari wanne wakamatwa Dar es salaam