Diwani wa kuteuliwa wa kaunti ya Vihiga katika Mkoa wa Magharibi nchini Kenya ametoweka baada ya kuposti kimakosa picha zake za utupu kwenye grupu la whatsApp, Ijumaa iliyopita.

Diwani huyo anayefahamika kwa jina la Rhoda Omufumu alipost picha hizo zinazomuonesha akiwa na mwanaume asiyefahamika, kwenye grupu la WhatsApp la Bunge Dogo la Kaunti hiyo majira ya saa 3 na dakika 12 usiku.

Ingawa diwani huyo ametoweka, amekuwa akitoa majibu kupitia kwa mwakilishi wake ambaye amedai kuwa picha hizo zilitumwa bahati mbaya na mtu ambaye alichezea simu yake na sio yeye kwani hajui kutumia vizuri vifaa vya kidijitali.

Mwakilishi huyo aliongeza kuwa Omufumu ni kiongozi kanisani hivyo hawezi kufanya kitendo hicho.

“Mtu alichezea simu yake… ni kiongozi wa kanisa ambaye hawezi kufanya vitu kama hivyo kwenye mitandao ya kijamii. Ameolewa na ana watoto wakubwa,” alisema mwakilishi wa diwani huyo.

Kutokana na picha hiyo, kumekuwa na shinikizo kubwa kwenye mitandao ya kijamii ikimtaka diwani huyo kujiuzulu mara moja nafasi yake.

Kwa mujibu wa gazeti la The Star la Kenya, Diwani mwenzake mwanamke, Maureen Ambasa amewataka madiwani wengine wa kike kukutana haraka leo kwa ajili ya kuunda kamati ambayo italichunguza kiundani suala hilo.

Mume wa Omufumu pia aliwahi kuwa diwani.

Bondia Thomas Mashali Afariki Dunia
Mmoja afariki baada ya basi, Lori kuteketea kwa moto