Bondia Thomas Mashali (kulia pichani) amefariki dunia usiku wa kuamkia hii leo jijini Dar es salaam.

Taarifa zilizothibitishwa na rais wa organization ya ngumi za kulipwa nchini (TPBO), Yassin Abdallah Ustadh, zimeeleza kuwa, chanzo cha kifo cha Mashali bado hakijafahamika.

Ustadh amesema alipopata taarifa za kufariki kwa bondia huyo ambaye aliwahi kuwika katika masumbwi ya kulipwa ndani na nje ya nchi, alilazimika kusaka uthibitisho kutoka kwa rafiki zake wa karibu, Cosmas Cheka pamoja na Karama Nyirawila.

“Nimejiridhisha kuwa ni kweli na ndio maana nimeamua kuzungumza na nyinyi ili kuutaarifu umma wa watanzania kuhusu kifo cha bondia huyu,” alisema.

Amesema kufariki kwa bondia huyo kumemsikitisha kutokana na ukaribu uliokua umejengeka baina yao.“Alinichukulia mimi kama baba yake wa hiyari na hata mimi nilimlea kama mwanangu wa hiyari.”

“Daima tutamkumbuka na tutaendelea kuuthamini mchango wake alioutoa katika masumbwi ya kulipwa hapa nchini na hata nje ya nchi.” Alisema Ustadh kwa njia ya Simu.

Mungu Ametoa Na Mungu Ametwaa Jina Lake Lihimidiwe.

Gareth Bale Kudumu Santiago Bernabeu Hadi 2022
Diwani apost picha zake za utupu kwenye grupu la Whatsapp la Bunge