Mshambuliaji wa pembeni kutoka nchini Wales, Gareth Bale amekamilisha mpango wa kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia klabu ya Real Madrid.

Bale mwenye umri wa miaka 27, amekubali kusaini mkataba wa miaka sita ambao utafikia kikomo Juni 30 mwaka 2022.

Bale alijiunga na mabingwa hao wa soka barani Ulaya, akitokea nchini England alipokua akiitumikia klabu ya Tottenham mwaka 2013, kwa ada ya uhamisho ya Pauni milioni 85.3 ambayo kwa kipindi hicho ilivunja rekodi duniani.

Taarifa iliyotolewa na klabu ya Real Madrid imeeleza kuwa: “Real Madrid na Gareth Bale tumesaini mkataba wa miaka sita, hivyo ataendelea kuwa hapa hadi Juni 30 mwaka 2022.

“Kesho (leo) saa 1:30 mchana, Gareth Bale atazungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa Santiago Bernabeu.”

Frank de Boer Kusubiri Hatma Yake Inter MIlan
Bondia Thomas Mashali Afariki Dunia