Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO, limeiwezesha serikali ya Lebonan kupata dozi 600,000 za chanjo dhidi ya ugonjwa wa Kipindupindu kutoka Kundi la kimataifa la uratibu wa chanjo za kipindupindu ICG, tayari kwa kampeni ya chanjo dhidi ya ugonjwa huo itakayoanza kesho Jumamosi Novemba 12, 2022.

Kwa mujibu wa Taarifa ya WHO, iliyotolewa hii leo Novemba 11, 2022 jijini Beirut Lebanon, imesema kampeni ya chanjo italenga wakimbizi na jamii zinazowahifadhi wenye umri kuanzia mwaka mmoja na kuendelea, ikilenga asilimia 70 ya wananchi na kila wiki watu 200,000 kupatiwa chanjo katika kipindi cha wiki tatu.

 Shehena ya kwanza ya vifaa tiba kupambana na kipindupindu iliyowasili nchini Lebanon. Picha ya WHO.

Mwakilishi wa WHO nchini Lebanon, Dkt. Dr Abdinasir Abubakar amesema, “Chanjo hizi zitakuwa nyenzo muhimu kuongeza nguvu katika hatua zatu za kukabiliana na mlipuko wa kipindupindu ambao unasambaa kwa kasi nchini humu.Kuwasili kwa chanjo hizi nchini ni hatua ya wakati na tunashukuru jitihada za pamoja kwa kushirikiana na wizara ya afya ya Lebanon mashirika ya umoja wa Mataifa na wadau wetu wengine nchini humu.”

Aidha, WHO imesema inagharamia dozi hizo 600,000 kutoka kwa ICG, ambayo inasimamia hifadhi ya kimataifa ya chanjo ya kipindupindu inayotolewa kwa njia ya matone mdomoni, na inatoa mwongozo wa kiufundi kuhusu uteuzi wa maeneo lengwa, uundaji wa mipango midogo midogo na mafunzo ya washirika wa utekelezaji wanaohusika na kutolewa kwa chanjo hiyo.

Samia aridhia Wanafunzi kuendelea na usajili
Viongozi wa Dini wakataa 'unafiki' wa Jumuiya ya Kimataifa