Mgombea wa Urais wa Tanzania kupitia chama cha NLD Maisha Mapya Muchunguzi leo agosti 19, 2020 amekabithiwa fomu za uteuzi wa Urais na mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi NEC, Jaji Semistoles Kaijage.

Muchunguzi amekuwa mgombea wa 17 kujitosa kwenye mbio hizo za kuwania kuteuliwa na NEC kugombea Urais katika uchaguzi mkuu wa tarehe Octobar 28 mwaka huu.

Vyama vyenye usajili wa kudumu Tanzania ni 19 huku vyama vya UDP na TLP havijajitosa kwenye kinyanganyiro hicho kwasababu vimekwisha weka wazi kumuunga mkono mgombea wa Chama Cha Mapinduzi CCM Rais John Magufuli.

Mpaka hivi sasa idadi ya wagombea waliojitokeza ni 17, kubwa ukilinganisha na uchaguzi wa mwaka 2015 ambapo waliochukua fomu walikuwa 11, walioteuliwa na NEC kugombea walikuwa 8, na wawili hawakurejesha fomu huku mmoja alilejesha fomu nje ya muda,

Sirro: Mwanasiasa muhalifu halali yetu
Leo tena donge nono- Waziri Mpango