Kocha wa muda wa timu ya taifa ya Uingereza Gareth Southgate, ametangaza kikosi cha wachezaji 23, tayari kwa maandalizi ya mchezo ya kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia dhidi ya Malta na Slovenia.

Mshambuliaji kinda wa Man Utd aliyetarajiwa kuitwa Marcus Rashford ametajwa kwenye kikosi hicho sambamba na Wayne Rooney, Daniel Sturridge pamoja na Jamie Vardy ambao kwa pamoja walikuwepo katika kikosi kilichotajwa kwa mara ya mwisho na kocha aliyetangaza kujiuzulu juma lililopita Sam Allardyce.

Beki wa pembeni wa Stoke city Glen Johnson naye ametajwa katika kikosi hicho ambacho kitacheza dhidi ya Malta Oktoba 08 na kisha Slovenia oktoba 11.

Kikosi kamili kilichotajwa na kocha wa muda Gareth Southgate .

Makipa: Fraser Forster (Southampton), Joe Hart (Torino, loan from Manchester City) na Tom Heaton (Burnley)

Mabeki: Ryan Bertrand (Southampton), Gary Cahill (Chelsea), Phil Jagielka (Everton), Glen Johnson (Stoke City), Danny Rose (Tottenham Hotspur), Chris Smalling (Manchester United), John Stones (Manchester City) na Kyle Walker (Tottenham Hotspur).

Viungo: Eric Dier (Tottenham Hotspur), Jordan Henderson (Liverpool), Alex Oxlade-Chamberlain (Arsenal), Michail Antonio (West Ham United), Jesse Lingard (Manchester United), Raheem Sterling (Manchester City), Theo Walcott (Arsenal) na Dele Alli (Tottenham Hotspur).

Washambuliaji: Wayne Rooney (Manchester United), Marcus Rashford (Manchester United), Daniel Sturridge (Liverpool) na Jamie Vardy (Leicester City).

Video: Nyoka apoteza maisha baada ya kung’ata ‘ziwa feki’ la mrembo kwenye tamasha
Gereza la kitengule Kagera, JPM aagiza wasipewe fedha yoyote watetemeke na kufanya kazi