Tukio la ajabu limeongeza hali ya tahadhari zaidi kwa wanawake wenye ndoto ya kuongeza ukubwa wa matiti yao kwa kufanya upasuaji na wanaume wanaotamani kuyatumia kwakuwa kinachowekwa ndani kubadili maumbile kinaweza kuwa sumu kali hata kwa nyoka.

Tahadhari imekuja baada ya nyoka aliyekuwa akitumiwa na mrembo mmoja kufanya onesho kupoteza maisha baada ya kupandwa hasira na kumng’ata mrembo huyo kwenye titi ambalo ni ‘feki’ lililotengenezwa kwa kutumia kemikali zenye silicon.

Kwa mujibu wa mtandao wa deccanchronic ulioweka sehemu ya Video ya tukio hilo, mrembo huyo anaonekana akicheza kwa mbwembwe na joka kubwa lililouzunguka mwili wake, lakini ghafla joka hilo lilipandwa hasira na kumng’ata kwenye titi. Kwa kawaida sehemu hiyo ilikuwa hatari zaidi kwa mrembo huyo lakini iligeuka kuwa hatari kwa joka hilo ambalo limeripotiwa kufa baadae.

Imeelezwa kuwa mrembo huyo alipata matibabu ya haraka kwa kuchomwa sindano mahususi za kuzuia kusambaa kwa sumu ya nyoka, lakini sumu ya silicon iliyokuwa kwenye titi lake feki iliyachukua maisha ya joka hilo.

Zinedine Zidane: Hakuna Baya Linaloendelea Kikosini
Gareth Southgate Awaita 23, Glen Johnson Arejeshwa Kundini