Penzi la msanii wa muziki nchini aliyefanya vizuri na kijiwe chake cha ”Papa”, Gigy Money na Moj 360 limesambaratika gafla mara baada ya mwanadada uyo kujifungua mtoto wa kike anayejulikana kama Myra.

Gigy Money amehojiwa na Clouds media na kufunguka wazi kuwa yeye na Moj360 ambaye ni mtangangazaji wa Radio ya Choice Fm, wameachana rasmi.

Gigy Money ametaja sababu kubwa kuwa baba mtoto wake kutomuheshimu kwani amekuwa akimdharau kwa kauli ambazo zimekuwa hazimpendezi mbali na hilo amesema wamekuwa wakigombana mara kwa mara hivyo ameona waachane kwani wanaume wapo wengi duniani, amedai Gigy.

”Kweli ni Ex wangu baba mtoto wangu, mzazi mwenzangu, kuna vitu vingine inabidi ukue kiakili na ukubaliane na hali halisi, na ujielewe, unaishi na mtu hamna tofauti na mwaka jana na mwaka juzi bado mtu anajiona yupo vile vile wanaume wote hawa duniani” amesema Gigy Money.

Hata hivyo Clouds Media ilimtafuta Moj 360 kuthibitisha hilo ambapo naye amesema ni kweli wameachana hivyo kwa sasa kila mtu aishi maisha yake.

”Mtoto wangu nampenda sana  na nitaendelea kumpenda tumuache yeye na maishi yake na mimi nibaki na maisha yangu”   Amesema Moj 360 akimaanisha Gigy aishi maisha yake naye aishi yake.

Hii ni hatari sana kwa mtoto, hata hivyo tabia ya wasanii kuzalishana na kubwagana imekithiri kupita kiasi, ifike mahala wasanii wajitambue kuwa wao ni kioo cha jamii hivyo matukio kama haya hubomoa jamii kwa namna moja au nyingine, na mara zote wanaoathirika zaidi ni mama na mtoto, wasanii wanapaswa kubadilika.

Harusi ya kifalme ya zaidi ya Sh. 100 bilioni kushuhudiwa kesho
Dkt. Possi awasilisha hati ya utambulisho kwa Papa Francis

Comments

comments