Msemaji wa klabu ya Simba, Haji Sunday Manara ameiomba mamamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA, imchukulie hatua shabiki wa Young Africans, Pascal Lameck aliyeposti kwenye mtandao wa kijamii wa facebook taarifa ya uongo kuwa basi la wachezaji wa Simba limepata ajali na wachezaji wote wamevunjika mguu, huku kocha wao, Joseph Omog akiwa hajulikani alipo.

Kupitia posti aliyoitoa kwenye mtandao wa facebook, Manara amehoji uhalali wa shabiki huyo kuendelea kuwepo uraiani akitazamwa bila ya kuchukuliwa hatua za kisheria na mamlaka ya mawasiliano ya TCRA.

“Always huwa najiuliza mashabiki wa aina hii tunawaacha kwa nini?  Na TCRA ichukue hatua, tusingoje hadi watukanwe wakubwa tu, hatuwezi kusamehe kila kitu,” ameandika Manara kwenye posti yake aliyoiambatanisha na posti ya shabiki huyo.

Picha: Waziri Mwigulu awasilisha makadirio ya Bajeti ya wizara yake
UVCCM yang'aka, yawaonya wasaliti ndani ya jumuiya