Mbunge wa Kawe, Halima Mdee amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu kwa ajili ya kusomewa mashtaka yanayomkabili baada ya kukamatwa na jeshi la polisi wiki iliyopita.

Mara baada ya kusomewa mashtaka, Mdee ameachiwa kwa dhamana ya Shilingi Milioni 10 pamoja na wadhamini wawili baada ya kusomewa shitaka moja la kutoa lugha ya matusi.

Mdee alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu hivi leo baada ya kukamatwa na jeshi la polisi wiki iliyopita,ambapo atarudi tena Mahakamani hapo 7 mwezi wa 8 mwaka huu.

 

VIdeo: Majaliwa awasili mkoani Lindi
Auwawa kwa kupigwa risasi Kibiti, mke ajeruhiwa vibaya