Hispania imekubali kuwapokea wahamiaji kutoka Afrika waliookolewa majini wiki iliyopita mara baada ya kukataliwa na nchi za Italia na Malta.

Wahamiaji hao ambao wengi wao ni kutoka nchini Libya wameorodheshwa kwa ajili ya kuanza kupatiwa matibabu na misaada mbalimbali ya kibinadamu.

Tukio hilo limezua mjadala mkubwa wa kisiasa barani Ulaya mara baada ya serikali ya Italia na Malta kukataa kuwapokea wahamiaji hao.

Aidha, Shirika la msalaba mwekundu limezitaka nchi za jumuiya ya Ulaya, kuiga mfano wa Hispania kuonyesha mshikamano katika suala la wahamiaji.

Hata hivyo, kwa upande wake Ofisa mkuu wa Uhamiaji na Polisi wa mpakani nchini humo, Bernardo Alonso amesema kuwa wahamiaji hao watapata haki zote za msingi wakiwa kama wakimbizi.

 

 

 

Chidi Benz atiwa mbaroni tena
Polisi washutumiwa kuomba rushwa ya kreti za bia