Leo, Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha inatarajia kutoa hukumu ya kesi dhidi ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake Sylvester Nyegu na Daniel Mbura wanaokabiliwa na mashtaka ya unyang’anyi wa kutumia silaha.

Awali, hukumu hiyo ilipaswa kusomwa Oktoba 1, 2021, lakini Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Amalia Mushi aliahirisha hadi leo, Oktoba 15, 2021 ambapo mbivu na mbichi zitajulikana.

Wakaazi wa Mkoa wa Kilimanjaro na Arusha wamefika mapema na kwa wingi katika Mahakama hiyo kwa lengo la kufahamu kitakachojili.

Sabaya na wenzake walikamatwa Mei 27, 2021 jijini Dar es Salaam na kufikishwa Mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Juni 4, 2021.

Upande wa Jamhuri ulikamilisha ushahidi wake kwa kuwasikiliza mashahidi 11 na vielelezo vinane.

Polisi mbaroni kwa kumsaidia mtuhumiwa wa mauaji kutoroka selo
Zaidi ya 85% ya visa vya Covid Afrika havijagunduliwa – WHO