Kundi la kigaidi la Islamic States (IS) limetoa taarifa jioni hii na kueleza kuwa ndilo lililohusika na mashambulizi ya kigaidi nchini Ufaransa yaliyosababisha vifo vya watu 127, Ijumaa usiku (Novemba 13).

Kundi hilo limekiri kuhusika na mashambulizi 6 katika maeneo sita tofauti katika jiji la Paris kuanzia majira ya saa tatu usiku.

Kwa mujibu taarifa zilizotolewa na maafisa wa Ufaransa, watu 99 walijeruhiwa katika matukio hayo ya kujitoa mhanga. Washambuliaji nane waliripotiwa kufariki, saba wakiwa wamejilipua kwa kujitoa mhanga. Inaelezwa kuwa passport ya Syria ilipatikana kati ya miili ya washambuliaji hao huku taarifa nyingine zikieleza kuwa raia wa Ufaransa pia alihusika katika mashambulizi hayo.

Ulinzi umeimarishwa jijini Paris

Ulinzi umeimarishwa jijini Paris

Washambuliaji walifanya mauaji katika tamasha la muziki wa rock, kwenye mgahawa maarufu, na uwanja wa michezo.

Nchi za Marekani, Sweden, Romania na Ubelgiji pia wameeleza kuwa raia wao waliathirika na mashambulizi hayo.

Rais wa Ufaransa, Francois Hollande ametangaza hali ya hatari katika nchi hiyo huku akiimarisha ulinzi mkali katika maeneo yote. Rais Hollande ametangaza siku tatu za maombolezo na kueleza kuwa kitendo hicho ni dhahiri kuwa IS imetangaza vita rasmi dhidi ya Ufaransa.

 

Mwanamke Aliyemuua Mwanae Kwa 'Kumuoka' Kwenye Oven Ahukumiwa
Watanzania Waishio Thailand Wachagua Viongozi Wao