Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Seleman Jaffo amesema kuwa waganga wakuu watakaoshindwa kutumia vizuri fedha zinazotolewa na mfuko wa basket fund, watafukuzwa kazi.

Jaffo ametoa onyo hilo Mjini Kibaha wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Kibaha Vijijini na Kibaha Mjini, kwenye mwendelezo wa ziara yake na kuzungumza na watumishi wa umma.

“Fedha hizo zinazotolewa kwaajili ya miradi ya maendeleo hasa katika ununuzi wa dawa kwenye hospitali na hata katika ujenzi wa majengo ya afya, lakini inaonekana kuna ujanja  wa watu wachache wanatafuna fedha hizo ambazo asilimia 33, ni kwaajili ya kununua dawa na zinazobaki zinatakiwa kukarabati majengo ya hospitali,”amesema Jaffo.

Pamoja na hayo, aliwataka Wakuu wa Idara kusimamia majukumu yao kikamilifu na kufanya kazi kwa weledi ikiwemo kuacha upendeleo wa kuwapandisha madaraja baadhi ya watumishi na kuwaacha wenye sifa.

Kwa upande wake, Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Happines William, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, amesema kuwa atahakikisha maagizo yaliyotolewa na Naibu Waziri huyo yanafanyiwa kazi ili waweze kwenda na kasi iliyopo Serikalini.

 

 

Timbulo: 'Usisahau' ingebuma nisingefanya muziki
MSD yawatoa hofu watanzania kuhusu hali ya dawa nchini