Mshambuliaji Jamie Vardy amerudisha kijembe kwa baadhi ya wadau wa soka ambao walikinyooshea kidole kikosi cha mabingwa watetezi nchini England Leicester City, kwa kusema kilichangia kutimuliwa kwa Claudio Ranieri juma lililopita kwa kufanya mgomo baridi.

Vardy amerudisha kijembe hicho, alipohojiwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini England, baada ya mchezo wao na Liverpool uliomalizika kwa majogoo wa Anfield kukubali kibano cha mabao matatu kwa moja.

Mshambuliaji huyo ambaye alifunga mabao mawili kati ya matatu yaliyoipa ushindi Leicester City, alisema haikupaswa kwa wachezaji kutupiwa lawama kwa kisingizio cha kutazamwa kama chanzo cha safari ya aliekuwa meneja wao.

Vardy alisema: “Tumekua katika hali ya kulaumiwa tangu alipoondoka Ranieri juma lililopita, lakini ukweli ni kwamba hakuna lolote lililofanywa na wachezaji, zaidi ya upepo mbaya uliokua umetukumba.”

“Leo (Jana) tumecheza vizuri baada ya kila mmoja wetu kutambua nini kilichokua kinahitajika, na huenda hili limetokana na maagizo tofauti tuliopewa na watu wa benchi la ufundi, ambao kwa mara ya kwanza hawakua na Ranieri.

“Hakuna aliyefurahia kuondolewa kwa Ranieri, kila mmoja alisikitika kwa sababu tuliishinae vizuri hadi kutwaa ubingwa wa EPL msimu uliopita, lakini hakuna nafasi ya kuendelea kulijadili hilo, kwani yaliyotokea, yametokea, na sasa tunaangalia namna ya kujitoa kwenye nafasi ambayo inahatarisha ushiriki wetu katika ligi kuu msimu ujao.”

Bao lingine la Leicester City kwenye mchezo wa usiku wa kuamkia leo lilifuingwa na Danny Drinkwater, huku Philippe Coutinho akiwafuta machozi Liverpool kwa kufunga bao pekee kwa wekundu hao.

Srivaddhanaprabha: Haikuwa Rahisi Kumfuta Kazi Ranieri
Dogo Janja amtumia ujumbe mzito Makonda