Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Simon Sirro amesema kuwa ushirikiano unaoendelea kutolewa na wananchi kwa jeshi hilo, umesaidia pakubwa kupunguza uhalifu kwa kiasi kikubwa nchini na kuongeza kuwa wamejipanga kuhakikisha Sikukuu ya Pasaka itasherehekewa kwa amani na utulivu.

Sirro amesema kuwa jeshi hilo limejipanga vizuri kuhakikisha wananchi wanasherekea sikukuu ya Pasaka kwa amani na utulivu.

Aidha, ameongeza kuwa kiujumla hali ya usalama ni shwari na matukio makubwa ya uhalifu wa kutumia silaha yamepungua kwa kiasi kikubwa, huku jitihada za kukabiliana na makosa ya usalama barabarani zinaendelea ili kupunguza ajali zinazosababisha vifo na majeruhi kwa raia.

Hata hivyo,amewataka wazazi kuwaangalia watoto wao na kuto waacha kutembea peke yao bila ya kuwa na uangalizi wa karibu, pia wamiliki wa kumbi za starehe wanatakiwa kufuata sheria, kanuni na taratibu za uendeshaji wa kumbi hizo ikiwemo kutoruhusu disko toto na kujaza watu kupita kiasi.

 

Miguna ajikuta yuko Dubai, aomba msaada wa matibabu
Magazeti ya Tanzania leo Machi 29, 2018

Comments

comments