Pamoja na kuongoza kwa kukusanya alama 56 katika Ligi ya Daraja la Kwanza Tanzania Bara ‘Championship’ na kukaribia kucheza Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao 2023/24, timu ya JKT Tanzania imeweka rekodi kadhaa nzuri ikiwamo kuongoza kushinda michezo mingi ugenini na nyumbani.

Kwa mujibu wa takwimu za ligi hiyo, JKT Tanzania ambao wameshacheza michezo 23, wakisalia na michezo saba tu, wameshinda mara 10 nyumbani kati ya michezo 12, huku wakishinda michezo minane ugenini kati ya michezo 11 ambayo wameshuka dimbani.

Wakati Maafande hao wakiwa vinara katika ligi hiyo, na kushinda michezo mingi ya nyumbani na ugenini, Kitayoce ya Tabora ambayo inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi hiyo wakiwa na alama 49, inaifuatia JKT Tanzania kwa kushinda michezo mingi nyumbani, imeshinda mara tisa kati ya michezo 11. Pamba inashika nafasi ya tatu kwa kufikisha alama 47.

Takwimu hizo zinaonyesha nafasi ya tatu kwa timu zilizoshinda nyumbani inashikiliwa na Mashujaa FC, ikishinda mara tisa kati ya michezo 12, Pamba FC wako katika nafasi ya nne wakicheza michezo 10 na kushinda minane huku KenGold wakimaliza tano bora kwa kushinda michezo minane.

Rais Samia azindua Kamati tathmini utendaji Wizara Mambo ya nje
Odds kubwa Wikiendi hii, Bayern vs Dortmund, Man City vs Liverpool