Baada ya kupoteza pambano la masumbwi dhidi ya Oleksandr Usyk, aliyekuwa bingwa wa uzito wa juu raia wa England, Anthony Joshua amesema atarudi ulingoni tena kumkabili mpinzani wake huyo ambaye ametwaa mikanda yote ya WBA, WBO na IBF aliyokuwa akiishikilia.

Joshua ambaye alipanda ulingoni usiku wa kuamkia Jumapili (Septamba 26) katika Uwanja wa Tottenham Hotspur, Uingereza katika pambano la raundi 12, amesema alipigwa na bingwa wa uzito wa juu raia wa Ukraine baada ya kupasuka juu ya jicho.

“Sikuweza kuona raundi ya tisa nilikuwa sioni kitu sababu jicho langu lilikuwa limefunga, nilitumia uzoefu sababu unapaswa kujifunza jinsi ya kujizuia mwenyewe katika mambo yote, hii ni mara ya kwanza kwangu kutokea nikiwa ulingoni.”

“Nataka kurudi gym napaswa kurudi chini na kuboresha uwezo wangu pindi nitakaporudi kumkabili bondia huyu mzuri, lilikuwa funzo nzuri kwangu, najua kila mmoja anaweza kulitafsiri hili kwa vile anavyoona, lakini kwangu nalichukua kama darasa ambalo limenijenga.”

“Mimi ni mnyama wa tofauti hii ni nafasi iliyobarikiwa  kwa kupanda ulingoni kucheza katika uzito wa juu, sirudi nyumbani kulia sababu hii ni vita na hili ni zoezi la muda mrefu sio pambano moja ambalo nimemaliza,” alisema na kuongeza.”

“Sitaki kumuangalia mpinzani wangu, nataka kujiangalia mimi nilikosea wapi, hakuwa bora ni nafasi niliyompa narudi kwenda kuangalia wapi nilipojikwaa na kurekebisha makosa.”

Promota wa bondia huyo, Eddie Hearn  alisema Joshua alimuheshimu Usyk mwenye umri wa miaka 34 ndio maana aliweka mikanda yake mitatu ya WBA, WBO na IBF ambayo aliipoteza baada ya kupasuka juu ya jicho lake.

“Sikuwahi kumuona Joshua akifikisha raundi 10, lakini katika miaka miwili ya karibuni labda hiki ndio kitu ambacho tunapaswa kukiangalia.”

Ramsey kuingizwa sokoni Januari 2022
Live: Rais Samia ashiriki Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Viongozi wa ALAT Taifa