Msanii wa maigizo ya Vichekesho, Lucas Mhavile maarufu kama Joti, ametoa ufafanuzi juu ya nyumba yake aliyokuwa anaijenga eneo la kibada Wilaya ya Kigamboni kuwekwa alama ya X ikimaanisha ipo mbioni kubomolewa.

Joti amesema Tanroads wanafanya utanuzi wa barabara ambapo hauhusiani na ubomoji wa nyumba, amesema nyumba yake haijakumbwa na bomoabomoa bali ni ukuta tu ndio utakaobomolewa ili kupanua barabara.

”Wanapanua barabara huku kwetu, lakini huu upanuzi wa barabara haujahusiana na ubomoaji wa nyumba, wengi wanajua nyumba yangu ndio inabomolewa lakini sivyo, kinachobomolewa ni ukuta tu” amesema Joti.

Mbali na Joti kuna wakazi wengine 130 kata ya Kibada na Kisarawe wamekumbwa na janga hilo ambapo Wakala wa Barabara Tanzania Tanroads, wameweka alama ya X katika nyumba hizo zilizopo barabarani.

Aidha Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa amewataka wananchi wote waliowekewa alama hizo kufika ofisini kwake, Mei 5, 2018 kwa ajili ya mazungumzo yatakayowakutanisha wataalamu wa Wizara, Tanroads na Manispaa ili kuona namna bora ya kutatua shida hiyo.

 

Acha watunyooshe tu maana tulizoea kuropoka- Lucy Mayenga
Ndalichako awaonya baadhi ya watumishi

Comments

comments