Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Magufuli ameviagiza vyombo vya dola, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kuchunguza mradi wa ujenzi wa jengo la ukumbi wa mihadhara na ofisi za Wahadhiri katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa (MUCE) kilichopo Manispaa ya Iringa.

Ametoa agizo hilo wakati alipotembelea chuo hicho na kuzungumza na wanafunzi na Wahadhiri katika uwanja wa michezo.

 “Chuo cha Mkwawa mnani-disappoint, ndiyo maana sikuja kuweka jiwe la msingi, siwezi kuweka jiwe la msingi kwenye jengo lililojengwa kifisadi. Kuna Profesa mmoja alikuja hapa mka-mretain, alitakiwa awe mahakamani, anaitwa Profesa Mushi,”amesema JPM

Amesema kuwa profesa huyo anahitajika kutafutwa hata kama amestaafu na anastahili kuwepo mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabiri.

Hata hivyo, ameagiza kuwa vyombo vinavyohusika vifuatilie kesi iliyofunguliwa dhidi ya Mkandarasi aliyekuwa akijenga majengo hayo.

Video: Wabunge CCM wataka mishahara iongezwe, JPM awapasha wabunge
Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Mei 3, 2018

Comments

comments