Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 15 Julai 2020 amefanya uteuzi wa viongozi wa Mikoa na Wilaya, akiwepo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Aboubakar Kunenge.

RC Kunenge anachukua nafasi ya Paul Makonda ambaye amechukua fomu ya kugombea Ubunge jimbo la Kigamboni, kabla ya uteuzi huo alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es salaam.

Rais Magufuli amemteua Joseph Mkirikiti kuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara, anachukua nafasi ya Alexander Pastory, na kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Hanang.

Paulo Makanza ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es salaam ambapo kabla ya uteuzi huo alikuwa Afisa Mwandamizi wa Benki kuu ya Tanzania (BOT).

Aidha Rais Magufuli amemteua Dkt. Seleman Serera kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma ambaye anachukua nafasi ya Deo Ndejembi, kabla ya uteuzi huo alikuwa Afisa Mwandamizi wa CCM Makao Makuu.

TFF, TPLB: Morrison hakufanya kosa
Lampard ahimiza mapambano Chelsea