Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amemteua Alphayo Kidata kuwa balozi ambaye atapangiwa sehemu ya kazi.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Ikulu, Balozi John Kijazi imesema kuwa uteuzi huo umeanza rasmi tarehe 10 Januari 2018.

Aidha, kabla ya uteuzi huo Alphayo Kidata alikuwa Katibu Mkuu Ikulu, huku akimteua Meja Jenerali Mstaafu, Simon Mumwi kuwa balozi.

Hata hivyo, wateule hao watapangiwa vituo vyao vya kazi na kuapishwa baada ya taratibu za kikazi kukamilika.

Kibatala ajiengua uwakili kesi ya Wema Sepetu
Wavaa nusu utupu kufikishwa mahakamani

Comments

comments