Aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini kupitia Chama cha NCCR-Mageuzi, David Kafulila baada ya kukabidhiwa kadi ya uanachama  wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo,amesema kuwa chama hicho ni cha mwendo kasi.

Kafulila ameyasema hayo mbele ya wajumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, muda mfupi mara baada ya kukabidhiwa kadi ya uanachama wa chama hicho.

Mwanasisa huyo aliyewahi kuwa mwanachama na kiongozi wa ngazi ya juu wa Chadema, kabla ya kutimkia NCCR-Mageuzi zaidi ya miongo miwili iliyopita, amesema kuwa kutokana na mwendo kasi huo chama hicho kinakwenda kushinda Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

“Ukiwa ndani ya gari au treni unaweza usione spidi yake, lakini ukiwa nje utaona spidi yake, mimi nilikuwa nje nimeona spidi ya Chadema,Mwenyekiti Mbowe nitume sehemu utakayotaka nitakwenda, nipo tayari kufungwa nina uchungu na Tanzania yangu,”amesema Kafulila.

Hata hivyo,mwanasiasa huyo alimpiga kijembe mwanasiasa mmoja aliyekuwa NCCR-Mageuzi aliyehamia Chama cha Mapinduzi (CCM), kuwa amepoteza mwelekeo.

Arsene Wenger: Sina Mpango Wa Kumsajili Payet
Lissu akana kuchapisha taarifa za uchochezi