Baraza la vyama Vya Soka Afrika Mashariki na Kati ‘CECAFA’ limethibitisha kuahirishwa kwa Michuano ya kuwania kufuzu katika Ligi ya Mabingwa ya Wanawake ukanda huo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) Auka Gecheo amesema maamuzi ya kuahirishwa kwa Michuano hiyo, yemetokana na Kenya kutarajia kuwa mwenyeji wa Michuano ya Riadha ya Dunia ya U20 2021 katika Uwanja wa Kasarani.

Gecheo amesema Shirikisho la Soka nchini Kenya (FKF) limewaarifu kuhusu taarifa hizo, na hawana budi kupanga tarehe nyingine ya kuanza kwa Michuano hiyo.

Awali CECAFA na FKF walitangaza Michuano hiyo ingeza kurindima Agosti 7-21, lakini sasa imesogezwa mbele hadi Agosti 24.

CECAFA ilikuwa imepanga Michuano ya kuwania kufuzu katika Ligi ya Mabingwa ya Wanawake ukanda huo ichezwe kwenye Viwanja vya Nyayo na Kasarani jijini Nairobi.

Mshindi kutoka ukanda wa CECAFA atacheza kwenye Ligi ya Mabingwa ya Barani Afrika ‘CAF’ ya Wanawake ambapo Misri itakua mwenyeji.

Haruna Niyonzima ataja anaowapenda Ligi Kuu
Young Africans, Morrison kumekucha CAS