Kocha wa timu ya taifa ya Togo Claude LeRoy amemuita mshambuliaji Emmanuel Adebayor kwenye kikosi cha wachezaji 22, kitakachokua na jukumu la kujiandaa viivyo kwa ajili ya mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Afika 2019, dhidi ya Algeria.

LeRoy amemuita mshambuliaji huyo, licha ya kukataa kucheza katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Afrika 2019 mwezi Oktoba dhidi ya Gambia, kwa kisingizio cha kutoridhishwa na mazingira ya uwanja wa nyasi bandia mjini Lome.

Wakati akitangaza kikosi LeRoy alisema, ameshazungumza na Adebayor na amemthibitishia kuwa tayari kucheza mchezo dhidi ya Algeria, kwenye uwanja wa mjini Lome, ambao alikataa kucheza mwezi uliopita.

Kocha huyo kutoka nchini Ufaransa pia amewaita kikosini wachezaji wanaocheza soka katika ligi ya Togo Ouro-Akoriko Sadate na Wilson Akakpo ili kuziba nafasi za Djene Dakonam na Ouro-Sama Hakim ambao wanatumikia adhabu ta kuonyeshwa kadi za njano.

Bila ya mshambuliaji Adebayor, Togo iliambulia matokeo ya sare ya bao moja kwa moja mjini Lome, na siku chache baadae waliibuka na ushindi wa bao moja kwa sifiri dhidi ya Gambia ugenini.

Matokeo hayo yaliiacha Togo katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa kundi D, baada ya kushika dimbani mara nne, huku wakizidiwa alama mbili na vinara wa kundi hilo Algeria na Benin.

Timu ya taifa ya Togo (The Sparrow Hawks) itahitaji ushindi dhidi ya Algeria ili kufanikisha azma ya kuongoza msimamo wa kundi D, ambalo kwa sasa linaongozwa na Mbweha wa Jangwani( Algeria).

Kikosi cha Togo kilichotajwa kwa ajili ya mchezo dhidi ya Algeria.

Makipa: Sabirou Bassa Djeri (Coton Sport, Cameroon), Malcolm Barcola (Olympique Lyonnais, France) na Fadil Soumanou (Koroki)

Mabeki: Ouro-Akoriko Sadate (Amazulu FC, South Africa), Simon Gbegnon (AS Beziers, France), Maklibé Kouloum (Dyto Lome), Tevi Steve Lawson (Livingstone, Scotland), James Olufade (Union Douala, Cameroon) na Wilson Akakpo (Al Ittihad, Egypt)

Viungo: Lalawele Atakora (FK Qabala, Azerbaijan), Koffi Franco Atchou (Fremad Amager, Denmark), Floyd Ayite (Fulham, England), Ihlas Bebou (Hannover 96, Germany), Razak Boukari (Chateauroux, France), Matthieu Dossevi (Toulouse, France) na Bilali Akoro (AS OTR)

Washambuliaji: Emmanuel Adebayor (Ä°stanbul Basaksehir, Turkey), Kevin Denkey (Nimes, France), Kodjo Fo-Doh Laba (Renaissance Berkane, Morocco), Peniel Mlapa (VVV Venlo, Netherlands), Bodzroma Jean (Koroki) na Gilles Sunu (Erzurumspor, Turkey)

Tiwa Savage aweka rekodi tuzo za ‘MTV EMAs’
LIVE: Msemaji wa Serikali akizungumza na waandishi wa habari