Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans Nasreddine Mohamed Nabi amesema anatamani kufanya kazi na Kiungo Mshambuliaji Simon Msuva, baada ya kumfuatilia na kuridhishwa na uwezo wake.

Msuva ambaye alikua anawatumikia Mabingwa wa Soka Barani Afrika Wydad Casablanca, kabla ya kuingia kwenye matatizo ya kudai maslahi yake, amekua nchini Tanzania kwa muda mferu akifanya mazoezi binafsi.

Kocha Nabi amesema Msuva ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa, na kama atabahatika kufanya naye kazi atafurahishwa sana na hatua hiyo, kwani anahitaji kuwa na mtu mwenye kaliba kama yake.

“Natamani sana kufanya kazi na yule Msuva (Simon), ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa. Napenda sana kasi yake, juhudi zake lakini kitu bora zaidi anaweza kufunga na kucheza nafasi nyingi. Nitafurahi viongozi wangu wakimpata.”

“Sisi ni mabingwa sasa hapa Tanzania, kwa sasa najua Msuva ana shida na klabu yake, najua yataisha ila wakati huu ni kitu kizuri angekuja hapa Young Africans aweze kupambana kujiweka sawa, atalisaidia taifa lake na hata sisi tutapata kitu.” amesema Kocha Nabi

Tayari Msuva ameshathibitishwa kufuatwa na viongozi wa klabu za Simba SC na Young Africans katika kipindi hiki cha usajili, ili akubali kujiunga na moja ya klabu hizo, ambazo zimedhamiria kuboresha vikosi vyao kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi Kuu na Michuano ya Kimataifa.

Simba SC yaangukia kwa Josef Vukuzic
Mzozo wa DR Congo na Rwanda wachukua sura ya mashauriano